Tuesday, 17 April 2018

SERIKALI YAAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO KWA WANAFUNZI WENYE UZIWI


Waziri wa Elimu, Sayasni na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amekihakikishia Chama cha walimu Viziwi kuwa Serikali iko tayari kusikiliza na kujua changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye uziwi ili hatua madhubuti ziweze kuchukuliwa.

Waziri Ndalichako amesema hayo leo mkoani Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na walimu wenye Uziwi  ambapo amewaeleza kuwa hajafurahishwa na matokeo ya kidato cha Nne ya shule ya Sekondari Njombe na kubainisha kuwa ni vyema changamoto zikaainishwa ili hatua ziweze kuchukuliwa.

 Kwa upande wake mratibu wa chama hicho cha Walimu  Viziwi Francis Mbisso ameiomba Serikali kutoa semina kwa walimu wanaofundisha wanafunzi Viziwi ili  walimu waweze kuelewa saikolojia ya wanafunzi pale wanapowafundisha, lakini pia kuwe  na wigo mpana  wa mafunzo ya ufundi kwa wanafunzi hao  badala ya kuwalazimisha kusoma masomo ya darasani.

Mbisso ameshauri kuwepo kwa mtaala wa lugha ya alama pekee utakaowasiadi wanafunzi wenye uziwi kuelewa kwa uarahisi masomo yao wanapokuwa darasani ikiwa ni pamoja na kuongeza muda ya kipindi darasani ukilinganisha na muda wanaotumia wanafunzi wa kawaida.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawsiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
16/4/2018Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba  Newsili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.


Tumekurahisishia; Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: