Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo imewafuta kazi Mahakimu 250 ambao hawana elimu ya sheria pamoja na wale ambao walikuwa wameshtumiwa kuwa mafisadi.

 Waziri wa Sheria Alexis Thambwe Mwamba amesema hatua hii imechukuliwa ili kuwazuia watu waliokuwa wanaingia katika idara ya Mahakama wakiwa na lengo la kujipatia fedha badala ya kuwatumikia raia wa nchi hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa serikali ya Kinshasa kuwachukulia hatua maafisa wa juu wa idara ya Mahakama, Mwaka 2009, rais Joseph Kabila aliwafuta kazi Majaji 96 baada ya kubainika kuwa walikuwa wafisadi.

Hatua hii inakuja ikisalia miezi 7 ili kufanyike Uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu
Share To:

msumbanews

Post A Comment: