Sunday, 8 April 2018

Sehemu ya Tano : LENGO LA SIRI (COVERT PURPOSE)MWANDISHI: INNOCENT MAKAUKI

INSTAGRAM: Makeynovels_tz
MOVIE SCRIPTS/ BOOKING YA KITABU: 0622088300

Inaendelea ilipoishia toleo lilopita.....

 ... Japo Naomi alijaribu kuulizia hiyo hali baada ya kugundua Job hakua na uchanga! mfu anaokua nao kila siku wanapokua pamoja lakini alimjibu tu ni uchovu na hangover ya jana.

Job akajiandaa vizuri pia Naomi, na kama saa moja baadae Job alikua akimshusha Naomi nje ya geti la Chuo kikuu cha Uhasibu Arusha (Arusha Institute of Accountancy) alipokua akichukua shahada ya pili ya uhasibu. "Masomo mema mpenzi" Job aliaga
"Asante baby.

Leo tuna vipindi vya jioni usije mchana hadi nikupigie simu"
"Sawa hata hivo leo nina kazi ngumu sana mchana nitapata muda zaidi wa kufanya vizuri" wakaagana kisha job akageuza gari kurudi mjini.

Ilikua ni dakika ishirini zimepita tangia itimie saa tatu asubuhi muda wa kukutana na mtu asiyejulikana asiye na jina hajui ni mweusi au mweupe ulikua unakaribia.

Cha msingi tu ni hakusahau bastola yake ndani ya koti ilikua imetulia na ikiwa haina upungufu wa risasi.

 Maswali yalikua mengi ikiwa ni miezi mitatu imepita akiwa anafanyia upelelezi mauaji ya waziri mkuu tena kwa umakini wa hali ya juu na akiwa amekuja jijini Arusha  tangu mauaji yalipotokea kwa kivuli cha mfanyabiasha.

Upelelezi ulio mgumu kuliko yote aliyokwisha kuifanya kwani umehusisha mambo makubwa, watu wakubwa na makundi makubwa yenye nguvu ndani na nje ya serikali. Pamoja na yote hii inakua simu muhimu na ya kipekee inayoweza kupelekea muuaji kujulikana pia watu wote waliosuka mpango mzima.

Baada mwendo wa dakika kumi na tano Job alikua akipaki gari yake kwenye moja ya garage iliyoko eneo la clock tower nje kidogo ya Jengo aliloelekezwa. Nia yake ilikua aende kwa miguu ili kuhakikisha hakuna mtu anaemfuata kabisa.

Hilo alifanikiwa isipokua sasa hivi yuko chini ya ulinzi bastola ipo chini na hajafanikiwa hata kugeuza shingo ajue ni nani. Sauti iliyokua kwenye simu ikizungumza kwa kutetema tena kwa kiingereza sasa ina ujasiri tena kwa kiswahili.

 Job hakufanya jaribio lolote bali kufuata maelekezo na kutembea hadi mbele ya bonnet ya Toyota V8 iliyokua mbele yake. "Zunguka upande wa pili wa gari alafu taratibu geuka kwangu" maelekezo yaliendelea wakati huu akisukumwa kidogo.

 Job akapiga hatua kadhaa na tayari ..

Itaendelea kesho
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: