Sehemu ya Saba : JINA LA RIWAYA: LENGO LA SIRI (COVERT PURPOSE)

MWANDISHI: INNOCENT MAKAUKI

INSTAGRAM: Makeynovels_tz
MOVIE SCRIPTS/ BOOKING YA KITABU: 0622088300

Inaendelea ilipoishia toleo lilopita.....

SEHEMU YA SABA

Mwingine aliyekua kwenye orodha ya Job alikua ni Waziri Mkuu Robert Kibwe aliyepata ajali mbaya yenye utata kisha kupigwa risasi mbili za kifuani na dereva aliyepigwa risasi moja utosini kisha zikaibiwa nyaraka muhimu za serikali na computer ndogo mali binafsi ya waziri. Akiwa bado anaangaliwa na mdomo wa bastola Job akafungua ukurasa unaofuata akiwa na shauku kubwa ya kuona kilicho ndani. Akakutana na picha kubwa juu iliyopigwa alama ya mkasi kwa kalamu nyekundu katikati ikiwa na jina juu Zabron Pima jina ambalo hakulitambua akainua shingo lakini kabla ya kuongea chochote akawahiwa "Ok. hilo file lina orodha ya watu wote waliokwishauawa na ambao wanafuata. Hili jambo ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri na nguvu kubwa ipo kwahiyo ni ngumu kulizuia kutokana na wahusika kuwa wamejipanga" jamaa aliongea akimwangalia Job kwa macho maangavu.
"Tuanze kwanza na jina lako halafu hiyo silaha sio muhimu sana" Job akarusha swali
"Unaeza ukaniita Mack. Ni Mwanajeshi mstaafu, muuaji niliyefunzwa na mdunguaji wa mbali a sniper. Na sitafanya unavyotaka najua ninachokifanya unisikilize kwa makini" Mack aliongea huku akiingiza mkono mmoja ndani ya mfuko wa koti huku mwingine ukiendelea kuishika bastola yake barabara. Akatoa picha na kuiweka juu ya bonnet na kuisogeza upande wa Job. "Anaitwa Gerald Marwa ni askari wa kimataifa INTERPOL raia wa Tanzania aliyekua mafichoni nchini Botswana. Wiki Sita zilizopita aligundulika kwenye maficho yake na kikosi maalum cha  Jeshi la serikali ya Africa ya kusini akihusishwa kushirikiana kundi moja la kihasi kupanga njama za kumuua kiongozi mwandamizi wa ngazi za juu kabisa wa serikali hiyo. Yeye  na mimi tumekua tukifanya kazi ndani ya kundi la PEMBE TATU au THE TRIANGLE. Sasa hivi yuko ndani ya gereza moja la kijeshi jijini pretoria nchini Afrika ya kusini. " Aliendelea kumpa Job taarifa zaidi zilizokua zinamfanya aendelee kusikiliza kwa makini na kujaribu kuunganisha matukio kujua uhusiano wa stori nzima anayopewa na mauaji ya waziri Kibwe, bado akiwa anaangaliana na mdomo wa bastola. "Sasa sikiliza kwa makini, kwa sababu hiki ndicho kipande muhimu na ndicho nilichokuitia hapa"

Huku akiingiza mkono mfukoni tena na kutoa simu yake na kufungua ujumbe mfupi ulioandikwa _SOWETO GROUNDS 09:30 PM_ kutoka kwenye namba ambayo ni private. Mack alimwonyesha Job huo ujumbe wote wakiwa kimya akairudisha simu mfukoni tayari kwa kulenga moja kwa moja kwenye kilichomleta hasa. Ukizingatia Job hadi wakati huu hajaweza kuunganisha matukio kutokana na maelezo ya Mack. Akaendelea "Huo ndio mfumo PEMBE TATU hutumia kuwasiliana na sisi, tumeshawahi kukutana na wenzangu wanaofanya kazi chini ya kundi hili ila hatujawahi kukutana na anayetoa maagizo yote. Kila tukio la kitaifa tunakuwepo bila kujua idadi yetu au kujuana kabisa ila kila mtu hufanya alichoagizwa na mwisho wa siku ni akaunti zetu za banki kujaa fedha za malipo. Kama unavyoona huo muda leo ni muda wa makutano na baadhi ya wajumbe wa juu wa PEMBE TATU na kwa taarifa nilizonazo ni kuhusu mwendelezo wa OPERATION D.O.A kama ilivyo ndani ya ilo file nililokupatia. Waziri mkuu alipogundua ndani ya serikali kuna kundi la maofisa katika vitengo nyeti kabisa wakishirikiana na viongozi wa juu ndani ya vikundi vya kigaidi na waasi kutengeneza serikali kivuli kwa ajili ya maslahi yaliyokua na maangamizi makubwa ndani yake, aliamua kuunda kikosi maalumu juu ya hilo na baada ya miezi miwili baadae alikabidhiwa ushahidi wa majina, barua pepe, picha za matukio unaowaanika wazi wahusika wakuu wa muundo wa PEMBE TATU na kazi ambazo kundi hili hufanya. Taarifa zilifika kwa uongozi wa kundi na hatimaye ikajulikana waziri mkuu alikua na huo ushahidi ndani ya msafara wake uliokua na magari matatu tu akielekea ndani ya kambi ya mafunzo ya Jeshi na msuko wa ajali ukafanyika, mauaji yakafanyika na ndipo nyaraka hizo zikaibiwa na kuwa mikononi mwa pembe tatu." Mack akaweka kituo.

Itaendelea kesho
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: