Sehemu ya Nne : Lengo la Siri - MSUMBA NEWS BLOG

Saturday, 7 April 2018

Sehemu ya Nne : Lengo la Siri


INSTAGRAM: Makeynovels_tz
MOVIE SCRIPS/KUFANYA BOOKING YA KITABU: 0622088300

Inaendelea ilipoishia toleo lililopita.....

SEHEMU YA NNE

"You have been working hard undercover to investigate who caused the accident and finally shot the minister and his driver in cold blood" sauti iliendelea Job akijiuliza maswali mengi.

Je huyu mtu ni nani? Amepataje kumjua hadi mawasiliano yake? Ni kwanini wakati huu? Ila yote hayakua na majibu. Hofu ilimtanda huku Naomi hajui chochote kinachoendelea anajigeuzageuza tu kitandani.

"I have some answers you want" Aliendelea
"Why do you think I want them. I'm not interested" Job alijibu akitia kiburi kidogo akijua kabisa hamaanishi anachokiongea alihitaji kujua kweli.

"Well. It's up to you. But you need the details indeed beuse they are coming for you anyway"

"Coming for who? For What? Who are they?" Job alijikuta akirusha maswali ya mfululizo akihisi nywele kumsimama na damu kuongeza spidi ndani ya mishipa yake kuliko kawaida.

Job alijua kabisa majibu ya maswali aliyoyauliza ila alitaka tu kujitia uhakika. Ila alichotarajia kusikia upande wa pili wa simu hakukipata badala yake alipewa maelekezo ya jinsi ya kukutana aweze kupewa hizo taarifa muhimu. Simu ilikatwa na kuachwa na bumbuwazi bila kujua cha kufanya.

Kikubwa alichoweza ni kufungua friji na kujitolea chupa Captain Morgan Jamaica Rum na kumimina nusu glasi kisha akaishusha kooni kama maji na hakuisikia hata inavopita kwa kuchoma kama wakati mwingine.

Kitu kingine ni kua wakati wote wa kwenda kwenye friji na kufanya yote Naomi alishaamka akajifunga taulo kiunoni akiacha sehemu kubwa ya matiti na mapaja meupe nje katika namna ambayo mwanaume yeyote rijali angetokwa na udenda hata kama ameishi nae karne nzima.

Macho ya kichokozi yaliyomlegea ilikua ndio risasi ya mwisho inayoweza kumuua tembo wa ukubwa wowote ule.

"Baby mbona umeamka mapema hivo" Naomi aliita kwa sauti ya kulalamika huku akimkumbatia Job kwa nyuma ila akili yake haikua pale na hilo alilidhihirisha kwa mshtuko aliouonyesha. 

Baada ya muda, wote walikua wameshaingia bafuni wakajipatia kifungua kinywa huku Job akijaribu kuonyesha kua kawaida bila kumwambia mpenzi wake Naomi kuhusu simu aliyopokea.....

Itaendelea kesho
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done