Tuesday, 17 April 2018

SEHEMU YA NANE: LENGO LA SIRI (COVERT PURPOSE)

MWANDISHI: INNOCENT MAKAUKI

INSTAGRAM: Makeynovels_tz
MOVIE SCRIPTS/ BOOKING YA KITABU: 0622088300

Inaendelea ilipoishia toleo lilopita.....
Mack akavuta pumzi kidogo kisha akaendelea. "Huyu alikua ni miongoni mwa watu muhimu sana katika usafirishaji wa mizigo muhimu ya kundi la PEMBE TATU, jina lake liliorodheshwa kwenye ushahidi aliokua nao waziri mkuu.

Tayari alishakua mzigo na angeweza kukamatwa na kuteswa na kutaja viongozi waandamizi wengine na kusababisha vita zaidi.

Yalifikiwa makubaliano kuwa aondolewe hivyo pia ile meli haikutekwa na waasi kama ilivyotangazwa kwenye vyombo vya habari na taarifa rasmi iliyotolewa na serikali.

Tukio zima lilisukwa na hatimaye mlinzi wa karibu kabisa wa Mr. Benson akamalizia tukio kwa kumlima risasi za ubongo bosi wake huyo na hadi sasa hajulikani alipo.

Zile silaha zipo mikononi mwa kundi dogo linalofanya shughuli zake nchini Somalia na Kenya pia Tanzania baada ya PEMBE TATU kutengeneza mahusiano ya karibu sana.

Gerald Marwa ndiye aliyekua kiungo muhimu wa makundi haya ndani na nje ya Tanzania na sasa ameshikiliwa huko Afrika kusini.

Ni mtu mwenye siri nzito ni lazima pembe tatu itafanya namna ya kumtorosha gerezani au kumuua kabisa kwa maana ni miongoni mwa watu wenye mafunzo ya hali ya juu sana sio rahisi kumdhuru bila tahadhari ya juu sana."

Wakati huu Job anashusha pumzi akigundua amejiingiza kwenye upelelezi hatari na mzito kuliko alivyodhani mwanzo.

Akigundua kila tukio lina mlolongo wa wahusika nyuma yake. Mack pia akirudisha bastola yake ndani ya koti baada ya maelezo yenye utata huku akimsisitiza Job kupitia orodha aliyompa kuunganisha dots ila pia asicheze mbali na viwanja vya SOWETO ambapo baadhi ya wadau wa PEMBE TATU wangekutana usiku katika muda uliokua kwenye ujumbe.

Katika hali hiyo hiyo alimwacha Job na kutokomea zake. Maswali aliyobaki nayo Job yalikua ni mengi ila mwanga na mwanzo umeshaanza kuonekana japo hakujua ni kwa nini Mack alimpa taarifa zote izo isije ikawa ni sehemu ya mpango. Kikubwa aliwaza kufanya hili kwa tahadhari ya hali ya juu sana.

Akiwa anawaza simu yake ikaita.

Job akapokea simu huku akiifadhi vizuri lile file alilopewa na Mack. Simu ilikuawa ni ya Director Wilson Gamba mkuu wa kitengo cha upelelezi makosa ya jinai Tanzania.

 Job na Director Gamba ukiachana na kuwa mtu na boss wake pia walikuwa marafiki wakubwa kwenye kazi na nje ya kazi.

Ni watu ambao wangekesha kwenye kupata mbili tatu lakini asubuhi Job anapiga saluti kama kawaida.

Dir.Gamba ndiye msimamizi mkuu na mshauri kwenye kazi zote alizowahi kuzifanya Job tangia atue nchini tokea Russia alipokua akimalizia masomo yake.

Dir.Gamba amekua mwalimu mzuri kwa Job hasa pale anapokuwa kwenye kazi nyeti kama upelelezi wa mauaji ya watu wazito namna hii.

Dir. Gamba alimpigia simu Job na kuuliza kama ameshasoma habari za kupatikana kwa mwili ya daktari aliyejulikana kwa jina la Dk. Damian Solomon.

Kwa habari zilizopo mwili wake ulikutwa kilomita kadhaa nje ya mapango yaliyopo milima ya Lengijave. Mapango ambayo kwa muda yamekua na matukio yasiyoisha ya kutisha na stori zake ni nyingi.

Wapelelezi kadhaa waliojaribu kuchunguza yafanyikayo humo na matukio yake hakuna ambaye ana taarifa za kurudi. Zimebaki kuwa stori tu za hapa na pale.

Dir. Gamba akiendelea kumlisha Job habari za kina kuhusu upatikanaji wa Dk. Damian, Job alikuwa akiongea nae huku naye akiwa ameshafika kwenye kibanda cha magazeti alichopita mwanzoni kabla ya kukutana na Mack.

Akawa anajipatia nakala yake ya Gazeti la Mwananchi iliyokuwa na kichwa cha habari na picha kubwa ya mwili uliofunikwa kwa shuka jeupe -MWILI WA DR. DAMIAN WAPATIKANA NJE KIDOGO MWA MAPANGO YA LENGIJAVE-.

Job akaondoka akiwa anamsikiliza Dk. Gamba akiwa ndo amefika kwenye kiini cha stori nzima.

"Siku moja kabla ya Dk. Damian kutekwa alitembelewa na Mwanake mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Maximillian na kuwa alikuwa akitaka kuonana na Dk Damian kwa ushauri juu ya magonjwa ya akili na matatizo saikolojia baada ya kusoma moja ya vitabu vyake. Wafanyakazi waliokuwa mapokezi walimuagiza huyo mwanamke iliko office ya Dk. Damian..

Itaendelea kesho
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: