Wednesday, 4 April 2018

SEHEMU YA 02 : "LENGO LA SIRI"

Mwandishi: Innocent Makauki
Instagram: @Makeynovels_tz

Magazeti mengi yalijaa habari za kisiasa na udaku wa wasanii wa muziki na filamu za kitanzania isipokua gazeti moja la kila siku la kiingereza liloonekana kuvuta umakini wa Job zaidi na bila kupoteza mda akatoa pochi katika mfuko wake wa nyuma na kutoa noti ya elfu mbili na bila kusubiri masalio yake akachukua gazeti  akapiga pafu ya sigara akaitupa na kusogea pembeni kidogo na kuanza kusoma.

 -THE PRESUMED MISSING DOCTOR FOUND DEAD- Kichwa kikubwa cha habari kiliandika huku mengine madogo yakisema -A journalist claims to have evidence on the group responsible- Job hakuendelea kusoma tena bali aliangalia tu kushoto na kulia na kuendelea na safari yake na baada ya dakika tatu za mwendo wenye ukimya na kutafakari alichokiona kwenye gazeti alikua akiingia ndani ya jumba moja lenye parking ya magari chini ya ardhi.

Job alipigiwa simu asubuhi na mapema na kua na ahadi ya kukutana na mtu humu ndani ambako taa zilizokua zikiwaka ziliionyesha vizuri gari nyeusi aina ya Toyota V8 iliyokua ni gari pekee iliyopaki humu ndani. Ukimya ulikua umetawala hakukua hata na sauti ya mdudu zaidi ya mwangwi wa viatu aina ya travolta alizovaa Job katika hatua alizokua akizipiga kuelekea lilipo gari.

Ghafla alihisi kufatwa kwa nyuma na kabla hajageuza shingo kuangalia alikua ashachelewa, kitu cha baridi kama mdomo wa chupa ya bia kilikua kimegusa uchogoni mwake akijua tayari yuko mbele ya mlango wa bastola ujanja ujanja wowote ungeweza ukamsababisha mwili na roho vikaachana huku ubongo ukiishia kua chakula cha sisimizi kwahiyo bila kujaribu kupiga hatua na mkono uliokua umewahi ndani ya koti kuwahi a.340 automatic pistol yake akiurudisha taratibu  kwa nidhamu ya hali ya juu. Sauti nzito ya mtu wa makamo isiyotetereka hata kidogo ikasikika

"taratibu toa bastola yako weka chini, ukijaribu chochote nakufumua ubongo" bila ubishia akaitoa akaiweka chini taratibu huku akinyanyuka "umeniita hapa kwa hili?" Job akauliza

"Huwa siweki imani yangu kwa watu kama nyie kirahisi. Tembea kuelekea lilipo gari mbele kabisa kwenye bonnet"
Job akaamriwa na kuanza kutembea huku akiwaza ni jinsi gani alichokitarajia kimegeuka kua dunia nyingine kabisa...
Itaendelea kesho

No comments:

Post a Comment