Wednesday, 18 April 2018

Sakata la RC Makonda: Kina Baba 540 wakubali kulea watoto, 60 kupimwa DNA


Idadi kubwa ya Kinababa walioitikia Wito wa kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda wamekubali kutoa matunzo ya mtoto huku wengi wao wakipongeza Zoezi hilo kwa kuweka mazingira bora kwa Mtoto.

RC Makonda amesema hadi kufikia jana Kinababa waliokubali kutunza watoto walifikia 540 na kinababa 60 walipimwa DNA ambapo amewapongeza wenza wote waliofika na kukubali kuwatunza watoto ambapo ametangaza vita Kali kwa wale wanaume watakaokaidi wito wa serikali.
Licha ya leo kuingia siku ya nane tangu lilipoanza, bado idadi kubwa ya kinamama wapya wameendelea kujaa Ofisini kwa RC Makonda ambapo amesema kila aliefika kwake atahudumiwa.
Hata hivyo RC Makonda amesema idadi ya wananchi waliofika ofisini kwake ni zaidi ya 17,000 ambapo idadi ya waliosikilizwa hadi kufikia Jana walikuwa Wananchi zaidi ya 5,024.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: