Tuesday, 17 April 2018

sababu za Ray Kigosi ‘kuzikacha’ tuzo za APA kutoka Ghana

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Ray Kigosi amefunguka sababu ya kutohudhuria katika utoaji wa tuzo za The African Prestigious Awards (APA) 2017.

Tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia April 15, 2018 mjini Accra nchini Ghana, Ray na Monalisa waliibuka washindi kutoka Tanzania.
Ray Kigosi amesema alishindwa kuhudhuria utoaji wa tuzo hizo kutokana alikuwa safarini nje ya nchi.
“Sikufanikiwa kuhudhuria kwenye Awards hizo kwa sababu niko South Afrika kikazi sina cha kuwalipa ndugu zangu zaidi ya kuendelea kuwaletea Watanzania kazi nzuri zenye viwango boraili tuendelee kuiletea heshima nchi yetu,” amesema Ray Kigosi.
Soma Pia; Monalisa, Ray Kigosi washinda tuzo nchini Ghana
Katika tuzo hizo Ray Kigosi alishinda katika kipengele cha msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa alishinda katika kipendele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: