Saturday, 7 April 2018

Rosa Ree ajisogeza kwa Wanigeria

Baada ya kurekodi na rapper Emtee kutoka nchini Afrika Kusini Emtee, Rosa Ree ameweka wazi mipango yake ya kufanya kolabo na wasanii wa Afrika.

Rapper huyo ambaye kwa sasa yupo Nigeria amesema hata nchini humo kuna uwezekana akafanya kazi na baadhi ya wasanii.

“Hata hapa pia nina mpango wa kukutana na wasanii fulani ni kwa sababu tunajuana kupitia watu wengine” amesema.

Kuhusu idadi ya kolabo za kimataifa amesema, “The so many lakini at least nimeweka moja wazi, mkae mkao wa kula na huku pia tunaomba tutarudi na kitu kikubwa,”.

Kolabo ya Emtee na Rosa Ree ikitoka itamfanya kufikisha kolabo mbili na rapper wa kiume baada ya ile aliyofanya na Khalighraph Jones kutokea nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment