Thursday, 5 April 2018

Roma Mkatoliki akabidhiwa cheti na BASATA


Rapa Roma Mkatoliki leo Alhamisi Aprili 05, 2018 amekabidhiwa cheti cha usajili kutoka BASATA hii ni baada ya kupewa masharti ya kufanya hivyo na Wizara ya Habari ili aweze kufutiwa adhabu yake ya kutojihusisha na muziki kwa miezi sita.

Roma akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa cheti hicho, amewashukuru watu wote walipaza sauti hadi kufutiwa adhabu hiyo, pia amewaasa wasanii wenzake kuchukua hatua mapema za kujisajili.

No comments:

Post a comment