Rc Makonda: Sina mpango wa Kugombea Urais...Lengo Langu ni Kumsaidia Magufuli - MSUMBA NEWS BLOG

Saturday, 14 April 2018

Rc Makonda: Sina mpango wa Kugombea Urais...Lengo Langu ni Kumsaidia Magufuli


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema matatizo ya wanandoa hayatakiwi kumuathiri mtoto kiasi cha kumnyima haki zake.

Amesema, hata kama mtoto amezaliwa nje ya ndoa, ana haki sawa na ndiyo maana sheria ya mtoto (ya mwaka 2009) haijasema ni mtoto yupi, bali inamgusa kila mtoto.

“Haijalishi mtoto amezaliwa na ‘house girl, sheria haibagui mtoto inawalinda watoto wote,” amesema

Ameyasema hayo leo Aprili 14, katika mahojiano maalumu yanayorushwa mubashara na televisheni ya TBC.

“Ajenda kuu tunayoizingatia ni haki ya mtoto. Watoto wote wa ndani na nje ya ndoa wana haki sawa,” amesema.

Kadhalika, amewataka viongozi wa dini kutoa mafunzo ya malezi na wajibu wa wazazi kwa watoto kabla ya kufikia hatua ya kufunga ndoa.

“Mapungufu yaliyopo katika sheria yanawafanya maofisa wa ustawi wa jamii waonekane hawafanyi kazi. Mapungufu haya ya kisheria yanawanyima kufanya kazi kwa ufanisi.” Amesema
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done