Monday, 16 April 2018

RC Makonda atoa ujumbe kwa Lulu ‘wanaokuombea mema wachache

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtakia heri ya siku ya mfanano wa kuzaliwa Elizabeth Michael (Lulu) huku akimwambia kuwa wanaomuombea mema wachache ila wenye nyuso za huzuni ni wengi.
Makonda ameeleza kuwa kwa kuwa Mungu ametenda basi watakuja na nyuso za furaha japo hazina mahusiano na mioyo yao.
RC Makonda ametoa ujumbe huo ikiwa leo, April 16, 2018 ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa na Kupitia ukurasa wake wa Instagram Majay ameandika;
Kumbe wanaokuombea mema wako wachache ila wenyenyuso za huzuni wako wengi japo hawamaanishi. Na kwakua Mungu ametenda basi watakuja tena na nyuso za furaha japo hazina mahusiano na mioyo yao. Kwakifupi hii ndiyo dunia ambayo Mungu amekuongezea tena mwaka wa kuishi. Happy birthday mwanangu
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: