Friday, 13 April 2018

Rc Makonda aeleza mafanikio zoezi la wanawake waliotelekezwaMkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema zoezi la kudai haki za watoto waliotelekezwa limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo kati ya kinababa 226 waliofika kutii wito wake takribani kinababa 205 wamekubali kwa maandishi kuwahudumia watoto wao na 21 wamepimwa DNA.

Makonda amesema tangu kuanza kwa Zoezi hilo zaidi ya kinamama 10,000 wamefika kupata huduma na Kati ya hao Kinamama 4,000 wamesikilizwa ambapo Makonda amesema lengo lake ni kuhakikisha kila aliefika anasikilizwa na mtoto kupatiwa bima ya afya Bure.Aidha Makonda amesema wiki ijayo itakuwa zamu ya kusikiliza upande wa kinababa waliolalamikiwa sambamba na mwendelezo wa kuwasikiliza kinamama waliosalia.
Pamoja na hayo Makonda ametoa angalizo kwa kinababa watakaokaidi wito wa serikali kuwa watakamatwa popote walipo.


Kwa upande wa kinamama wanaopatiwa huduma wamemshukuru  Makonda kwa kutambua kilio chao ambapo wameonyesha kushangazwa na baadhi ya watu wanaobeza Zoezi hilo ambalo kwao wamesema limewasaidia kupata haki zao na kupata uhakika wa matibabu ya mtoto kupitia kadi za bima za afya zinazotelewa na  Makonda Bure.

No comments:

Post a Comment