Rasmi: Alikiba kuoa usiku wa leo

Msanii wa muziki Bongo, Alikiba anatarajia kuoa usiku wa leo.

Kwa muijibu wa Pilipili FM, Alikiba anafunga ndoa na mpenzi wake, Aminah Rikesh, Mombasa nchini Kenya.
Mama wa Bibi Harusi amesema; “Tunasherekea harusi ya mtoto wangu anaolewa na Alikiba, tunashukuru Mwenyenzi Mungu atupe furaha, anayepanga ni yeye hakuna anayeweza kupangua hata kama Alikiba ametoka TZ lakini Mungu ndiye ameshapanga”.

Licha ya wawili hao kufanya siri mahusiano yao hadi kufikia hatua ya kuoana, taarifa za ndani zinadai kuwa Alikiba na Aminah wameanza kuwa pamoja tangu mwaka 2016
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: