Friday, 6 April 2018

Rais Magufuli kuzindua ukuta wa madini ya Tanzanite Mererani leo


Rais John Magufuli leo Ijumaa Aprili 6, 2018 anazindua ukuta unaozunguka mgodi wa madini ya Tanzanite eneo la Mererani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.

Kukamilika kwa ujenzi wa ukuta huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Magufuli aliyoyatoa Septemba 2017 na kuliagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kujenga ukuta ndani ya kipindi cha miezi sita.

Jana, Msemaji Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Ramadhan Dogoli amesema ujenzi huo umekamilika na leo kiongozi mkuu huyo wa nchi atazindua.

Usipitwe na Habari Yoyote. Install Msumba news App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

No comments:

Post a Comment