Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pohn Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa nyumba za polisi na vituo vya polisi Jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wahabari Kamanda wa polisi jijini hapa DCP Charles Mkumbo amesema kuwa kutakuwa na uzinduzi wa vituo viwili cha Utalii na Diplomasia na kingine ni Kituo cha daraja la kati kilichopo Murieti Jijini Arusha.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa kutakuwepo pia na maonyesho mbalimbali ya jinsi Jeshi la Polisi linavyofanya kazi za kuwahudumia wananchi ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid .

Amewataka wananchi kutokuwa na hofu kwani hali ya usalama Jijini hapa umeimarishwa na amewaomba wajitokeze  kwa wingi katika sherehe hizo.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Msumba News App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

Tumekurahisishia; 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: