Friday, 6 April 2018

Rais Magufuli awataja wanaochonganisha nchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameweka wazi kuwa hatua inazopiga serikali kudhibiti uchumi, waliokuwa na tabia za kutuibia rasilimali hawawezi kufurahia, hivyo watatumia njia yoyote kukwamisha ikiwemo kuchonganisha.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akihutubia umma wakati wa uzinduzi wa ukuta uliojengwa kuzunguka eneo lenye madini ya Tanzanite, ambayo yanapatikana Tanzania pekee .
Rais Magufuli amesema watu hao wakiwemo wale waliokuwa wanaiba wanyama na kuwasafirisha kwa ndege ili miaka ya baadaye wasiwe na sababu ya kuja Tanzania kutalii, watatumia mbinu yoyote kuhakikisha Tanzania haifanikiwi kujikwamua kiuchumi, ili waje watawale tena.
Awamu ya tano inapambana vita ya uchumi, vita ya uchumi ni ngumu, inapambana na mabeberu ya kila aina, tunaowazuia wizi hawawezi wakafurahi, tunapowazuia wizi wa dhahabu hawawezi wakafurahi, waliokuwa wanasafirisha wanyama wetu kwenye ndege wakiwa hai ili miaka ijayo wasije hapa kutalii, hawawezi wakafurahi. Na ni watu wenye uwezo mkubwa, mengine ni mataifa makubwa kutoka nje, wataleta vitimbwi vya kila aina, watawachonganisha kwa kila aina, kwa sababu ukitaka watu uwatawale ni kuwachonganisha”, amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameendelea kwa kusema ...”wapo waliokuwa wanataka nchi yetu isiendelee, unanunua ndege, wanatumiwa watu wanashangilia kukamatwa ndege yao, ni ushetani kweli kweli, ndege ni yenu, mtapanda wote lakini mtu anasimama pale anasema afadhali imeshikwa, ibaki huko huko, mnajiulizaje mtu wa aina hiyo, mali ni yenu, imeshikwa ni mali yenu lakini wanashangilia.
Sambamba na hilo Rais Magufuli amewataka watanzania kuwa wazalendo na kuzingatia uchumi wa nchi, na sio kushangilia pale panapotokea tatizo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: