Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limewataka wananchi wa Mkoa wa Tabora  kuendea kusherehekea sikukuu ya Uhuru  kwa amani na utulivu na limetoa onyo kwa  wananchi wa Mkoa huu wenye mpango wa kuandamana waache mara moja kwani Jeshi la Polisi Mkoani hapa liko imara na limejipanga kukabiliana na yeyote atakayeleta uvunjifu wa amani. Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora SACP WILBROD MUTAFUNGWA wakati akiongea na waandishi wa habari.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: