Polisi afukuzwa Kazi kwa tuhuma za ubakaji


Jeshi la Polisi mkoani Lindi, limemtimua kazi askari wake wa kituo cha wilaya ya Ruangwa, H.1302 Bariki Michael {28} kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 14 (Jina limehifadhiwa kwa maadili).

Hayo yameelezwa na Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo mkoani hapa, SSP Renatu Chalya alipokuwa anazungumza na mwandishi wa habari Ofisini kwake na kusema mtuhumiwa huyo tayari amefikishwa Mahakamani akikabiliwa na Shitaka hilo, na kwa sasa yupo mahabusu akikabiliwa na shitaka hilo.

"Tayari tumeshamaliziana na askari Bariki Michael kwa kumtimua kazi ndani ya Jeshi. Unajuwa Jeshi letu la Polisi halitetei na kulea askari wasio na nidhamu", amesema Kaimu Kamanda Chalya.

Kwa upande mwingine, Kaimu Kamanda Chalya amesema mtuhumiwa huyo atapandishwa tena Mahakamani mnamo Aprili 14, 2018 ili aweze kusomewa shitaka linalomkabiri dhidi yake.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: