Leo April 30, 2018 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linaloendelea mjini Dodoma; Hizi ni baadhi ya picha ya yaliyojiri katika bunge hilo.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha kwa Wizara hiyo kwa mwaka 2018/19 Bungeni mjini Dodoma mapema leo

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akitoa maelezo Bungeni mapema leo kuhusu mikakati ya Serikali kuhusu kufikisha umeme katika vijiji vyote hapa nchini

Mbunge wa Mwanga Prof. Jumanne Maghembe akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuhusu mikakati inayoweza kusaidia kuendelea kukuza kiwango cha elimu hapa nchini

Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa akijibu swali Bungeni mjini Dodoma kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kujenga miundo mbinu hapa nchini

Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza jambo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo mjini Dodoma

Wageni mbalimbali walihudhuria Bunge wakiwemo Skauti wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu mapema leo Bungeni mjini Dodoma
Share To:

msumbanews

Post A Comment: