Friday, 20 April 2018

Picha: Makamu wa Rais katika ufunguzi wa Mkutano wa CHOGM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) ambapo anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mkutano huo ambao Kaulimbiu yake ni “Kuelekea Mustakabali wa Pamoja” unafanyika chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Mhe. Theresa May na umefunguliwa na Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza hapo jana April 19, 2018.
Majadiliano ya Mkutano wa CHOGM 2018 yatajikita kwenye maeneo manne makuu ya kipaumbele ambayo yatajadili namna Jumuiya ya Madola inaweza kufikia mustakabali wenye ustawi zaidi; mustakabali endelevu zaidi; mustakabali wenye haki zaidi; na mustakabali wenye usawa zaidi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May muda mfupi kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Mkutano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland muda mfupi kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Mkutano.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: