Friday, 27 April 2018

Picha: Kim Jong-un akutana kwa mara ya kwanza na Rais wa Korea Kusini

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amekutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in kwenye eneo la mstari wa kijeshi uliowekwa kuyagawa mataifa hayo mawili tangu vita vya Korea mwaka 1953.
Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN, limemnukuu msemaji wa Rais Korea Kusini, Yoon Young-chan, akisema kuwa kikao hicho cha viongozi hao wawili kimedumu kwa dakika 100.
Yoon ameongeza kuwa mkutano huo ambao unaajenda kuu tatu utaangazia masuala ya nchi hizo mbili ikiwemo silaha za nyuklia na kuboresha mahusiano, na kutafuta makazi ya amani rasmi.
Mwishoni mwa mwezi March mwaka huu Kim Jong-un alifanya ziara nchini China na kukutana na Rais Xi Jinping mjini Beijing. Hiyo ilikuwa ziara yake ya kwanza kufanya nje ya taifa lake la Korea Kaskazini.

Ujumbe aliouandika Kim Jong-un kwenye kitabu cha wageni

Kim Jong-un akisaini kitabu cha wageni wakati Rais Moon Jae-in akiwa amesimama pembeni yake

No comments:

Post a Comment