Mbunge wa Kawe Halima Mdee leo April 3, 2018 amefikiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi, ameomba kufanya marekebisho ya hati ya mashtaka ili kumuunganisha Mbunge huyo.

 Mdee alikamatwa juzi katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere(JNIA) akitokea Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa.

 Awali, viongozi sita wa Chadema, akiwamo Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, walisomewa mashtaka manane, yakiwamo ya uchochezi na kuhamasisha maandamano.

Lakini Mdee hakujumuishwa katika hati hiyo ya mashtaka  na hivyo Wakili Nchimbi ameiomba leo Aprili 3, kumuunganisha Mdee katika kesi hiyo.

Viongozi hao walitakiwa kuwa huru kwa dhamana tangu Machi 29 lakini wakaendelea kubaki mahabusu   baada ya kushindwa kusaini bondi ya Sh20 milioni.

Machi 29,  Hakimu Wilbard   Mashauri aliamuru kuwa viongozi hao wafikishwe mahakamani leo na kusaini bondi hiyo ndipo suala la rufaa lifanyiwe kazi. 



Share To:

msumbanews

Post A Comment: