Saturday, 14 April 2018

Pep Gurdiola kufufukia kwa Tottenham leo

Pep Gurdiola ametoka kupitia kipindi kigumu sana katika wiki mbili zilizopita, wametoka kupoteza mechi tatu na hii leo wakipoteza itakuwa ya nne, City hawajawahi kupoteza mechi nne mfululizo tangu mwaka 2006.
Manchester City katika michezo miwili iliyopita nyumbani kwa Tottenham wamepoteza yote, tena wakipoteza kwa jumla ya mabao 6 na wao wakipata bao moja tu, japo zote zilikuwa White Art Lane.
Tangu Tottenham walipopoteza mchezo dhidi ya Man City katika dimba la Etihad mwezi December, Tottenham hawajawahi kupoteza mchezo katika michezo yao 14 ya ligi iliyofuata (wakishinda michezo 11 na suluhu 3).
Christian Erikssen anaonekana wa moto akiwa ametoka kufunga katika mechi 3 mfululizo za Tottenham na Tottenham wakishinda mchezo wa leo itakuwa timu ya 8 Epl kushinda michezo 900 ya ligi.
Tayari Pep Gurdiola amezifunga Arsenal na Chelsea ugenini, katika historia ya Epl ni Blackburn Rovers, Charton na Coventry ndio vilabu pekee ambavyo vimewahi kuzifunga Arsenal, Chelsea na Tottenham nyumbani kwao katika msimu mmoja.
Tayari Sergio Aguero ana mabao 199 kwa City, na amewahi kuwafunga Tottenham mabao 10, anatafuta bao lake la 200 kwa Man City japo hajawahi kuwafunga Tottenham katika michezo yao mitano ya mwishoo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: