Naibu Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mh:Wiliam Olenasha amesema kuwa vyama vya upinzani siyo tasisi za kudumu kwasababu vimeanza kutetereka licha ya kupata ruzuku kila mwezi havina ofisi rasmi kwa ajili ya wananchi wao.

Akizungumza mwishoni mwa wiki hii mkoani mkoani Arusha Olenasha ametolea mfano wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema ambapo amesema kuwa chama hicho kwa mwezi kinapata ruzuku ya shilingi milioni 400 lakini hawana ofisi hata ya shilingi elfu kumi.

“CCM ni tasisi ya kudumu wakati vyama vya upinzani kwa kweli siyo tasisi za kudumu yani tumendelea ukiona kwamba vyama vya upinzani vimendelea kutetereka ni kwasababu hazikuundwa ili zidumu na ndiyo maana kwa mfano chadema chama ambacho kimesajiliwa na kimeanza kufanya siasa kuanzia mwaka 1992 mpaka leo hii hawana ofisi hata ya shilingi 10000 sasa mtu kweli ambaye amedhamiria kudumu yani kuja kuongoza taifa hili ambaye ana malengo ya muda mrefu na anapata ruzuku ya shilingi milioni 400 kwa mwezi hawana hata ofisi hawajajenga hata ofisi nimefurahi nimeenda kwenye ofisi kata ya Levolosi chadema hata taifa hawana ofisi kama hiyo kimsingi ni njia ambazo zimetengenezwa kunufaisha watu wachache”Alisema Olenasha

Hata hivyo amesema kuwa anafurahi kuona chama mapinduzi ni tasisi ambayo ina jumuiya ambazo zimeundwa kwa ajili ya kusaidia jamii na amefarijika sana.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: