Monday, 16 April 2018

Nyota ya Msuva yazidi kuwaka Morocco

Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva usiku wa jana ameibuka shujaa wa timu yake ya Difaa Hassan El Jadida, baada ya kufunga mabao mawili ambayo yaliisadia kutoa sare ya 3-3 ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco dhidi ya Olympique de Khouribga.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya nchini Morocco. Msuva alifunga bao la kwanza katika dakika ya 65 huku bao la pili akifunga dakika ya 90+2, bao ambalo lilikuwa la kusawazisha na kuiokoa timu yake kuondoka na kichapo.

Bao la kwanza la Difaa Hassan El Jadida lilifungwa na Tarik Astati dakika ya 33. Mabao ya Khouribga yamefungwa na Zouhair El Moutaraji mawili dakika za nne na 38 na Adam Nafati dakika ya 55.

Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Jadida na kushuka kwa nafasi moja hadi ya nne kwenye Ligi ya Morocco yenye timu 16, ikifikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi 25.

Msuva amekuwa akifanya vizuri nchini Morocco akiwa kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya klabu ya Difaa iliyomsajili majira ya kiangazi akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Yanga SC.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: