Monday, 2 April 2018

Njombe Mji FC waahidi kuiyaibisha Simba

Kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Simba, Uongozi wa Njombe Mji umesema timu yao ipo tayari kwa mapambano.

Katibu Mkuu wa timu hiyo, Obed Mwakasungura, amesema wameshajiandaa kikamilifu kwa ajili ya kuikabili Simba.

Aidha, Mwakasungura amewaomba mashabiki wa Njombe Mji FC kujitokeza kwa wingi  ili kuipa hamasa timu yao.

Mwakasungura anaimani watapambana ili kupata ushindi japo amekiri kuwa mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa kila timu imejipanga.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: