Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes imeondoka nchini alfajiri ya leo kuelekea DR Congo tayari kwa mchezo wa marudiano kuwania kufuzu AFCON huku ikiwa na kazi ya kuhakikisha inafunga mabao.

Msafara huo umejumuisha wachezaji 21 na viongozi saba, ikiwa kamili kwaajili ya mchezo wake huo dhidi ya vijana wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Baada ya kufika Ngorongoro Heroes inayofundishwa na kocha Amy Ninje, itafanya mazoezi leo jioni pamoja na kesho asubuhi ambapo itafanya mazoezi ya mwisho tayari kwa mchezo utakaochezwa Jumapili Aprili 22,2018.

Kabla ya safari kocha Ammy Ninje amesema maandalizi yanaridhisha na vijana wamepokea vyema mafundisho yake ikiwemo mfumo mpya wa namna ya kucheza na DR Congo ugenini.

Endapo Ngorongoro itaibuka na ushindi na kusonga mbele, itakuwa imetinga hatua ya pili ya michuano hiyo ambapo itasubiri kupangiwa timu ya kucheza nayo na endapo itashinda mchezo huo itakuwa imefuzu kwa fainali hizo za vijana Africa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: