Wednesday, 11 April 2018

Mwili wa Mtanzania Aliyeuwawa Uingereza kukaa mochowari kwa siku 28


IKIWA leo ni siku ya 13 tangu mtanzania aliyeuawa na mumewe, Kema Salum, nchini Uingereza, Taarifa  zilizotufikia zinasema kuwa bado mwili wake unaendelea kuzuiliwa na jeshi la polisi nchini humo kwa ajili ya uchunguzi zaidi kutokana na kifo hicho tata.

Ripota wa wetu kutoka nchini Uingereza, Amuri Musema, anatuarifu kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakisubiri kwa hamu kupata taarifa kamili ni siku gani mwili wa Leyla utakabidhiwa kwa ndugu zake, lakini kuna taratibu mbalimbali za uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na vipimo ambapo nchi za Ulaya hufanya wakati mtu anapopatikana ameuawa kwa njia yoyote.

Wapo baadhi ya watu wa karibu na marehemu walioruusiwa kwenda kuuona mwili wake ambao wametibitishiwa kuwa ndio yeye na wamepewa taarifa kwamba ndani ya siku 28 kuanzia siku walipouona mwili huo ndio watakabidhiwa.

chanzo : Global Tv
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: