Saturday, 14 April 2018

Mwili wa mama wa Mrisho Gambo kuwasili Jumanne ijayo....Mazishi Alhamisi


Mama wa Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo anatarajiwa kuzikwa Uru mkoani Kilimanjaro baada ya mwili wake kurejeshwa nchini.

Katibu Tawala Mkoa Arusha, Richard Kwitega alisema hayo wakati akizungumza katika dua maalum leo, Aprili 14, iliyofanyika nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa.

Kwitega amesema, mwili wa  marehemu Rehema Momburi, unatarajiwa kuwasili Jumanne kutoka nchini India.

Kwa mujibu wa ratiba, mazishi yatafanyika Alhamisi  ya wiki ijayo.

Viongozi mbalimbali wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa, umoja wafanyabiashara, wakurugenzi, mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema na viongozi wengine kadhaa walihudhuria.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: