Mwenyekiti UVCCM: Simfahamu Mtu Anayejiita Mange Kimambi


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), (UVCCM), Kheri James amefunguka na kusema yeye hamtambui wala kumjua mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi na kusema angekuwa anamtambua angeweza kumzungumzia.

Kheri James amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa na kituo cha  EATV.

Mbali na hilo Kheri James alidai kuwa yeye hatambui wala kufahamu juu ya maandamano ya nchi nzima ambayo yanahamasishwa kupitia mitandao ya kijamii ambayo yanadaiwa kufanyika April 26 mwaka huu.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Kheri James amewalalamikia baadhi ya watanzania na wapinzani ambao wamekuwa wakiisema na kuitangaza nchi kwa mambo mabaya yaliyopo ndani

Amesema  jambo hilo ni baya sana kwani litaleta athari kubwa kwani wawekezaji, watalii watahofia kufika nchini  kwetu jambo ambalo litafunga milango ya maendeleo ya nchi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: