Mwandishi,Wahariri Waitwa Bungeni KuhojiwaSPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amemtaka mwandishi wa gazeto ;a Raia Mwema, Paschal Mayalana wahariri wa chombo hicho kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge ili kuhojiwa kwa madai ya kulidhalilisha Bunge.

Ndugai ametoa wito huo leo Aprili 12, 2018 Bungeni mjini Dodomawakati akitolea maamuzi mwongozo wa Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga, aliouomba Bungeni kulitaka lichukue hatua kwa kile alichokieleza kwamba gazeti hilo limechapisha makala yenye mlengo wa kulidhalilisha Bunge hilo.

Inadaiwa kwamba, Mayala aliandika makala kwenye gazeti hilo toleo la Aprili 9, 2018iliyosema “Bunge Linajipendekeza kwa Serikali.” Aidha, Ndugai hakutaja wanahabari hao wafike lini mbele ya kamati kwa ajili ya kuhojiwa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: