Monday, 2 April 2018

Mtulia, Mollel kuapishwa mkutano wa 11 wa Bunge unaoanza Kesho


Wakati kesho Aprili 3, 2018 ukitarajiwa kuanza kwa mkutano wa 11 wa Bunge utakao malizika Juni 29, 2018 Mjini Dodoma.

Wabunge wateule wawili kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni, Maulid Mtulia (Kinondoni) na Dk. Godwin Mollel (Siha), wanatarajia kuapishwa hiyo kesho.


Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Bunge Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, wabunge hao wateule wataapishwa katika Mkutano wa 11 wa Bunge utakaoanza kesho Jumanne Aprili 3, Mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya mijadala na kupitisha Bajeti ya Serikali na kujadili hotuba ya hali ya uchumi wa taifa itakayowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango.

Aidha, Bunge litajadili utekelezaji wa bajeti za wizara zote kwa mwaka wa fedha 2017/18 na makadirio ya matumizi ya Serikali kwa mwaka huo wa fedha.

Wabunge hao watakaoapishwa kesho, awali walikuwa wabunge kabla ya kujiuzulu na kuhamia CCM, ambapo Maulid Mtulia alikuwa Chama cha Wananchi (CUF) huku Dk. Mollel akiwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: