Friday, 6 April 2018

Mtibwa Sugar Fc kuikabili na Singida United Leo


Kikosi cha Singida United leo kinashuka dimbani kuikaribisha Mtibwa Sugar Fc katika mchezo wa ligi kuu bara.

Singida inaingia kucheza kibarua hicho ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata matokeo dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Mtibwa nao watacheza mchezo huu huku Simba ikiwasubiria mjini Morogoro katika mechi ijayo ya Ligi itakayopigwa Jumatatu ya wiki ijayo.

Tayari timu zote zimeshajiandaa na tambo zimeshatoka kwa pande zote mbili kuelekea mchezo huu utakaoanza saa 10 kamili jioni.

Mbali na mechi hiyo, Mbao FC nayo itakuwa inawaalika Lipuli FC kutoka Iringa. Mchezo huo utapigwa Kirumba Stadium jijini Mwanza saa 10 ya leo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: