Msigwa : Prof. Kitila Kasahau kazi yake anakazana kuwajibu Maaskofu


Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, amesema ili kujenga taifa lenye nguvu ni lazima kuwepo na hoja zinazokinzana huku akiwataka watendaji wa Serikali kufanya kazi za kuwatumikia wananchi.

Mch. Msigwa ameyasema hayo Bungeni jana wakati akizungumzia masuala ya Utawala Bora nchini na kudai kuwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, ni kama amesahau kazi yake na badala yake kutumia muda mwingi kuwajibu maaskofu.

“Badala ya kumtua mama ndoo, Prof. Kitila Mkumbo amekazana kuwajibu maaskofu ambao wanashughulika na roho za watu,” alisema Msigwa.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 komentar: