Sunday, 8 April 2018

Moto wawaka katika jengo la "Trump Tower"

Moto wawaka katika jengo la "Trump Tower" ambapo nyumba na ofisi za Donald Trump zinapatikana na kusababisha kifo cha mtu mmoja mjini New York.

Kwa mujibu wa habari,moto huo umeanzia katika ghorofa ya 50 ya jengo hilo.

Polisi mjini New York wameripoti kuwa mwanamume mwenye umri wa miaka 67 alifikishwa hospitalini lakini haikuwezekana kuyaokoa maisha yake.

Timu ya zima moto yenye watu takriban 200 ilifikishwa katika eneo la tukio ili kusaidia kuuzima moto huo.

Hata hivyo rais Donald Trump katika mtandao wake wa Twitter ameandika kuwa moto umedhibitiwa na kuwashukuru wote waliojitahidi kupambana na moto huo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: