Sunday, 15 April 2018

MONALISA AREJEA NCHINI NA TUZO YAKE


MSANII wa Bono Movies, Monalisa amejea nchini alfajiri ya leo Jumatatu, Aprili 16, 2018 akitokea Ghana ambako ameshinda Tuzo ya Filamu.
Monalisa amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere – Dar, akiwa na Tuzo yake ya Best African Female Movie Star 2018 ambapo alikuwa akishindanishwa na wasanii kutoka Ghana na Nigeria na aliwaburuza.
Mashabiki na Mastaa kibao wamejitokeza kumlaki Monalisa Airport wakiwemo Riyama, Wema, Davina na wengine.
Katika tuzo hizo, Ray Kigosi nae ameibuka mshindi wa Best African Male Movie Star 2018.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: