Mmiliki wa mabasi ya SabeAjipiga Risasi - MSUMBA NEWS BLOG

Wednesday, 11 April 2018

Mmiliki wa mabasi ya SabeAjipiga Risasi


Mfanyabiashara na Mmiliki wa mabasi ya HBS na Sabena, Sultan Hemed amejiua kwa kujipiga risasi asubuhi ya leo Aprili 11, 2018 nyumbani kwake Sikonge mkoani Tabora.

Akithibitisha taarifa hizo mbele ya waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa marehemu amejipiga risasi mdomoni na kutokea nyuma ya kichwa.

“Tumepokea taarifa za kifo cha mfanyabiashara ambaye ni mkazi wa wilaya ya Sikonge, ambaye anaitwa Sultan Hemed  mmiliki wa mabasi ya HBS leo asubuhi majira ya saa tatu amejipiga risasi nyumbani kwake. Risasi ambayo imeingilia mdomoni na kutokea nyuma ya kichwani,“amesema Kamanda Mutafungwa.

Hata hivyo, Kamanda Mutafungwa amesema kuwa jeshi la polisi limefika eneo la tukio kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadae.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done