Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza kimevunjika baada ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo na wataalamu wake kususia kikao hicho kwa kile kinachodaiwa kuwa sheria, kanuni na taratibu za kikao hicho zimekiukwa.

Hayo yamejiri kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe cha robo ya pili ya mwaka ,ambacho kimeshindwa kuendelea na majadiliano mara baada ya madiwani katika kikao hicho kuwasilisha hoja ya ukusanyaji wa mapato na ucheleweshaji wa vikao lijadiliwe kama suala la dharura ndani ya kikao hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw. Frank Bahari amesema kwamba Mwenyekiti wa halmashauri hiyo George Nyamahakwa kushinikiza kuendelea na kikao hicho ni kukiuka sheria kanuni na taratibu.

Hatua hiyo imechangia Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo pamoja na wataalamu wa halmashauri hiyo kutoka nje na kususia kikao hicho wakidai kutoridhishwa na hali ya uendeshaji wa kikao hicho.

Kutokana na malumbano hayo yanayoathiri maendeleo ya wananchi wa halmashauri hiyo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Frank Bahati amesema malumbano ya muda mrefu yatafanya halmshauri kushindwa kupanga mipango ya maendeleo kama hawatokubaliana.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo amedai kuwa malumbano hayo ya muda mrefu ndani ya halmashauri hiyo yamekuwa yakiwaadhibu wananchi wao na kuwataka madiwani hao wasifanye kazi kwa kutetea maslahi ya watu wachache.

Baraza la Madiwani  la  Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza  limedaiwa kwamba ni miongoni mwa mabaraza yanayoongoza kwa mivutano ambayo inadaiwa  chanzo chake ni maslahi binafsi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: