Tuesday, 24 April 2018

Mke mtarajiwa wa saba wa Jacob Zuma ajiuzulu kazi Afrika Kusini

Mwanamke ambaye anatarajiwa kuwa mke wa saba wa aliyekuwa rais wa Afrika kusini,Jacob Zuma, Nonkanyiso Conco amejiuzulu kazi nchini Afrika Kusini.
Jumamosi iliyopita Nonkanyiso (24) ambaye hivi karibuni alizaa mtoto wa kwanza na Zuma, alitangaza kujiuzulu mpaka ifikapo Jumatatu ya April 23.
Conco analazimika kujiuzulu cheo chake akiwa ni afisa mawasiliano wa kampeni ya kukabaliana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa wanawake wadogo, unyanyasaji wa kijinsia na ujauzito kwa watoto wadogo.

                                          Nonkanyiso Conco
Leonora Mathe ambaye ni naibu mwenyekiti wa shirika hilo, amethibitisha kuwa Conco ameandika barua hiyo. Hata hivyo mpaka sasa hajazungumza chochote juu ya uhuma hizo za kuhusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Zuma.
Wakati huo huo mrembo huyo anafanya kazi nyingine kwenye asasi inayohamasisha kampeni ya kuwawezesha mabinti wadogo katika maisha yao ya kila siku na kuacha kuwategemea wanaume wenye umri mkubwa.
Taarifa za Jacob Zuma na Nonkanyiso Conco kuwa na mahusiano ya kimapenzi zilianza kusambaa Ijumaa ya wiki iliyopita

No comments:

Post a comment