Tuesday, 24 April 2018

Miradi 33 kuboresha Halmashauri ya Jiji la MwanzaNa James Timber,
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeandaa mpango mkakati wa miaka mitano ya uwekezaji kimtaji ambao umeandaliwa kubainisha miradi 33 ya kiuwekezaji.

Akizungumza na Wandishi wa Habari mapema hii leo Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza James Bwire, alisema kuwa maandiko ya miradi 14 tayari imewasilishwa katika mfuko wa maendeleo ya kimtaji wa kimataifa ambapo tayari imeshafanyiwa kazi.

"Tunataka kuboresha stendi ya mabasi ya Nyegezi iwe na muonekeno wa Kimataifa pia Buhongwa kutajengwa eneo maalumu kwa ajili ya kuegeshea magari makubwa ambayo hayataruhusiwa kuingia mjini, huku  masoko ya biashara yatajengwa Nyegezi Buhongwa na Igoma," alisema Bwire.

Pia alisema mikakati mingine ya miradi hiyo ni kujenga uwanja wa mchezo wa Nyamagana kwa kiwango kinachotakiwa na kuweka vitu vya msingi kwa lengo la kuboresha sekta ya michezo jijini hapa.

Aidha alieleza mikakati ya  mradi katika eneo la Karakana ambapo patajengwa eneo la kuegeshea magari sambasamba na ujenzi wa eneo la michezo mbalimbali ya watoto ikiwa ni pamoja na eneo la kupumzikia.

No comments:

Post a Comment