Wednesday, 11 April 2018

Mch. Msigwa amvaa Jerry Muro, ni tuhuma za kumtelekeza mtoto


Mbunge wa Iringa mjini kupitia tiketi ya Chadema, Mch. Peter Msigwa amezidi kukana madai ya kumtelekeza mtoto na kueleza kuwa taarifa hizo zinaenezwa na Jerry Muro.
Akizungumza na EATV, Mch. Msigwa amesema kuwa madai hayo hayana ukweli wowote na kueleza iwapo lisemwalo lipo basi muhusika amtafute katika namba aliyoitoa na ikishindikana amfuate Bungeni.

“Mimi nitamtambuaje huyo mtoto, hiyo picha wameweka tu, ilipoanzia ni kwa Jerry Muro ndio ameanza kusambaza hizo habari kwamba mimi ni mwanamke aliyeenda kwa Makonda amejieleza ndio nimemuacha,” amesema Mch. Msigwa.

“Ninachokijibu pale, nakijibu kitu ambacho ameanzisha Jerry Muro, kwamba kuna mtu nimemtelekeza amekuwa akinitafauta na nimekuwa nikimzuia, nimejibu kwamba kama huyo mtu huyo yupo nimekuwa nikitoa namba zangu za simu na kama sipatikani aje hapa Bungeni,” amesisitiza.

Kuanzia mwanzo mwa wiki hii mamia ya wanawake walijitokeza ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili kupata msaada wa kisheria baada ya kutelekezwa na wazazi wenzio. Pia RC Makonda ametoa nafasi ya kuwasikiliza wanaume waliotelekezwa na wake zao ambapo watapatiwa msaada wa kisheria
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: