Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Nyamagana  na Taasisi ya First Community ya jijini hapa wametoa msaada wa mashuka 100 katika hospitali ya Butimba iliyopo katika Wilaya ya Nyamagana, yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 4.

Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula, Kelebi Luteli alisema Ofisi ya Mbunge imetoa msaada huo ili kupunguza changamoto, pia wanampango wa kuongeza majengo katika  vituo vya afya kwa lengo la kupunguza mlundikano hosptalini hapo.

Naye Katibu wa taasisi hiyo Flora Magabe alisema wao wameguswa hasa kwenye kipindi hiki cha zawadi za pasaka kuungana na wagonjwa na kuwapatia faraja kwa misaada hiyo ikiwa ni mwendelezo wa kutembelea makundi yenye huitaji.

"Sisi kama taasisi tumeguswa na watu waliosahaulika na wenye uhitaji ni vyema tukiwapa kidogo tulichonacho wapate faraja na wasione kama wametengwa," alisema.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo John Chagula alisema hospitali hiyo  inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa wodi ya wanaume jambo ambalo linafanya wagonjwa wa kiume kupata adha kubwa pindi wanapofika hapo kwa ajili ya kupata matibabu.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Butimba Yusuph Mgoyi alisema kuwa ukosefu wa wodi hiyo inaleta adha kwa wagonjwa wa kiume ikiwa na halmashauri kupoteza mafuta kwa kusafirisha wagonjwa hao kwenda kwenye hospitali ya mkoa Sekoutoure
Share To:

msumbanews

Post A Comment: