MBUNGE wa Rombo, Joseph Selasini, ameitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya Cyprian Musiba, akidai kuwa amekuwa akiitisha mikutano na waandishi wa habari na kuwashutumu baadhi ya viongozi na kutoa kauli kwamba angekuwa yeye angeweza hata kuua.

Selasini ameyasema hayo jana Aprili 11, 2018, Bungeni Mjini Dodoma na kumuomba Waziri mwenye dhamana ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, kulichukulia hatua gazeti linalomilikiwa na mtu huyo.

Aidha, Selasini amesema kwa hali ilivyo sasa, matukio ya watu kupotea na kuuawa, halafu Musiba anasema hadharani kuwa angekuwa yeye angeua na Serikali inamsikia na haimchukulii hatua, hali hiyo inampelekea kujenga hoja kwamba, Serikali imemtuma mtu huyo na kwamba ni mtu wao, vinginevyo watoe taarifa juu ya mtu huyo kuwa ni nani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: