Monday, 30 April 2018

Mbunge Mlinga aitaka Serikali kutochukulia shule za private kama adui


Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga ameihasa serikali kutochukulia shule za private kama adui yaani kama Chadema na CCM.

Mlinga ameyasema hayo leo Bungeni wakati akitoa maoni ya Kamati kwenye Wizara ya Elimu ambapo amesema kuwa kumiliki shule za private ni sawa na kupita na mihadarati kituo cha polisi.

“Tumeshuhudia zaidi ya asilimia 60 wanapata division four na division zero sasa nilikuwa noamba mtumie nguvu kubwa katika kuwekeza katika vyuo vya ufundi kwa hii miaka minne ambayo mtu anasoma kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne tungewekeza kwenye ufundi angeweza kuarchieve kitu kikubwa,“amesema Mlinga.

“Nataka niihase serikali yangu, serikali yangu tunazichukulia shule za Private kama adui yaani tunavyoichukulia Chadema na CCM na ndio serikali na shule za private, imekuwa kumiliki shule ya private ni sawa na kupita na mihadarati katika kituo cha Polisi. 

Naomba niwatoe hofu serikali mitaala mnatunga nyinyi, mitihani mnatunga nyinyi, tarehe ya kufanya mitihani mnatunga nyinyi, kusimamia mnasimamia nyinyi, mitihani mnasahihisha nyinyi na matokeo mnatangaza nyinyi hofu yenu nini na shule za private, fanyeni vizuri hizi shule za private zitakufa zenyewe naomba Mh. Waziri azingatie maoni ya Kamati hoja yake ni nzuri sana tangu nimfahamu waziri hotuba hii ni ya kwanza good endelea hivyo hivyo.“

No comments:

Post a Comment