Mbowe, Mashinji, watinga polisi na Kuachiwa......Mbunge Esther Bulaya amebaki Mahabusu - MSUMBA NEWS BLOG

Friday, 13 April 2018

Mbowe, Mashinji, watinga polisi na Kuachiwa......Mbunge Esther Bulaya amebaki Mahabusu


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk. Vincent Mashinji wameondoka katika Kituo Kikuu cha Polisi central baada ya kuripoti, huku Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya ikidaiwa atalala mahabusu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.

Wengine waliondoka kituoni hapo ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mashinji amesema kuwa wameripoti kituoni hapo kama walivyoamriwa na mahakama, lakini wameambiwa Mbunge Bulaya atabaki mahabusu kwa ajili ya upelelezi.

“Mbunge Bulaya amebaki mahabusu kwa sababu za kiupelelezi lakini tumeambiwa ataunganishwa katika shauri letu,” -Dk.Mashinji.
Comments


EmoticonEmoticon

Notification
This is just an example, you can fill it later with your own note.
Done