Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowet amempongeza Fatma Karume kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa TLS.

“Ushindi wako umetuma ujumbe kuwa mawakili wa Tanganyika wanajua msimamo wako na wanaamini kwa dhati kuwa kwa kushirikiana na viongozi wenzako mliochaguliwa kuongoza TLS utawavusha katika kipindi hiki ambacho Taifa linapitia na kushuhudia majaribu mengi ya uvunjifu wa Katiba, sheria na kanuni mbalimbali.

"Umepokea kijiti katika wakati ambao mtangulizi wako (Tundu Lissu) yuko hospitalini baada ya jaribio la shambulizi lililolenga kumuua kushindikana.

 “Tukutie moyo kuwa CHADEMA kama taasisi ya kisiasa tukiwa wadau wa masuala ya haki, sheria na utawala bora tuko nawe na tutaendelea kukupa ushirikiano wakati wote wa uongozi wako, wewe na wenzako wote.” -Mbowe 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: