Wednesday, 25 April 2018

Mbaya wa Buffon achaguliwa kuchezesha fainali ya FA

Refa ambaye alizua gumzo kwenye hatua ya robo fainali ya pili kati ya Real Madrid na Juventus, Michael Oliver amechaguliwa kuchezesha fainali ya kombe la FA.
Oliver aliteka vichwa vya habari April 11 kwenye mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabéu kwa kuipatia Madrid penalti dakika za mwisho pamoja na kumpatia kadi nyekundu kipa Gianluigi Buffon.
Refa huyo atachezesha mchezo huo wa fainali ya FA ambao utawakutanisha Manchester United na Chelsea.
Mchezo huo utachezwa Jumamosi ya Mei 19 ya mwaka huu kwenye uwanja wa Wembley.

No comments:

Post a Comment