Saturday, 14 April 2018

Matokeo ya Epl Man City Kishinda dhidi ya Tottenham

Liverpool 3-Bournemouth 0. Mo Salah amefunga bao 1 wakati Liverpool ikiwafunga Bournamouth mabao 3 kwa 0, bao hilo la Salah linamfanya kuwa Muafrika wa kwanza kufunga mabao 30 katika msimu mmoja wa ligi hiyo.
Lakini Salah pia anakuwa ameifungia Liverpool mabao 40, hii ikiwa mara ya pili kwa mchezaji kutoka Epl kufunga mabao 40+ katika msimu mmoja tangu Cristiano Ronaldo afanye hivyo msimu wa 2007/2008.
Chelsea 3-2 Crystal Palace. Shukrani kwa Olivier Giroud aliyeingia akitokea benchi kwani tayari Chelsea walikuwa wamekufa 2, lakini wakasawazisha na kushinda, kocha wa mwisho wa Chelsea kufanya “come back” ya namna hii alikuwa Claudio Ranieri.
Kwa sasa Giroud anakuwa na mabao 6 akitokea benchi msimu huu na ndio kinara wa watokea Sub, na toka ajiunge EPL ana mabao 19 akitokea sub ikiwa ni mabao 6 nyuma ya Jermain Defoe mwenye 25.
Crystal Palace 3-Brighton 2. Wilfred Zaha aliwafungia mabao 2 Palace katika ushindi wa leo, katika msimu huu wa ligi kuu nchini Uingereza hii ni mara ya kwanza kunafungwa mabao 5 katika kipindi cha kwanza cha mechi.
Tottenham 1-Man City 3. Sasa Manchester City wanakuwa timu ya 4 katika historia ya Epl kuwahi kuzifunga Arsenal, Chelsea na Tottenham katika viwanja vyao vya nyumbani ndani ya msimu mmoja, wengine waliowahi kufanya hivyo ni Blackburn Rovers, Charton na Coventry.
Kwa mara ya kwanza tangu kipigo kutoka kwa Leicester City cha mabao 4-3 mwaka 2015, hii leo kwa mara ya pili Tottenham Hotspur wanakubali tena kuruhusu mabao 3 katika uwanja wao wa nyumbani.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: